top of page

MIMBA ZA UTOTO 4,000 ZARIPOTIWA KILOSA

  • Khalidi
  • Jan 16, 2018
  • 1 min read

Mimba za utotoni 4,186 sawa na asilimia 30 ya wajawazito waliohudhuria kliniki, zimeripotiwa wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa kipindi cha mwaka jana.

Mbali ya hiyo, kesi za wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na ujauzito zimeripotiwa kuwa 15.

Meneja wa shirika la World Vision, Faraja Kulanga, alisema wamelibaini tatizo hilo kutokana na kukusanya takwimu za maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Kulanga alisema kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya watoto, hasa mimba na ndoa za utotoni, itasaidia kuwafanya watoto wa kike kufikia malengo yao ya maisha.

Alisema shirika kwa kuona ukubwa wa tatizo, liliamua kupita na kuchunguza chanzo cha wingi wa watoto kupata mimba, jambo ambalo linapaswa kupata ufumbuzi wa haraka.

Kulanga alisema kesi za mimba zinazoripotiwa kwa shule sekondari n inane, saba saba zikiripotiwa kwa shule za msingi.

Naye ofisa usitawi wa jamii Wilaya ya Kilosa, Tumaini Mohammed, alisema kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, Shirika la World Vision limekuja na mradi wa kupiga vita ukatili kwa watoto wadogo.

Aliwaomba wananchi wilayani humo kushirikiana na serikali kutoa taarifa kwa vyombo vya dola juu ya wazazi au mzazi anayeozesha mtoto aliyechini aliyechini ya miaka 18.

“Msikae kimya kuona mtoto wa jirani yako amepewa mimba, wakati uajua anasoma, lete taarifa tufanye kazi ya sheria ifuate mkondo wake,” alisema tumaini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi, alisema kampeni hiyo imekuja wakati mwafaka, hivyo kuwataka viongozi wa ngazi ya vijiji, kata hadi wilaya kushirikiana na shirika hilo.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page