top of page

ZAHANATI YAFUNGIWA KWA KUKOSA MHUDUMU.

  • khalidi
  • Feb 16, 2018
  • 1 min read

Zahanati ya kijiji cha mkola, halmashauri ya wilaya ya tandahimba mkoani mtwara, ambayo inatoa huduma katika vijiji vitatu imefungwa baada ya muugzi aliyekuwepo kwenda likizo ya uzazi kwa zaidi ya miezi minne sasa.

Akisoma taarifa ya kata ya lugalakatika kikao cha baraza la madiwani wilayani humu, diwani wa kata hiyo, ponella harid abdallah (CUF) alisema amelazimika kutoa taarifa hiyo ili mkurugenzi wa halmashauri ya tandahimba , said msomoka awasaidie kupata muuguzi.

Alisema amelazimika kufikisha ombi hilo baada ya kuona wananchi wa vijiji vya luagala, mkola juu na mkola chini wanapata adha ya huduma za matibabu kwa muda mrefu.

Abdallah alisema hivi sasa imepita miezi mine wakazi wa vijiji hivyo, hawapati huduma ya afya ipasavyo hali ambayo inawalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Hili tatizo ni la muda kituo kina muuguzi mmoja tu ambaye tangu achukue likizo ya miezi minn sasa, zahanati imefungwa na ni hatari inawezekanaje zahanati ihudumie vijiji vine iwe na mhudumu mmoja? Hili nalo ni tattizo alisema”

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page