LECHANTRE MIEZI SITA INAKUTOSHA SIMBA
- khalidi
- Jun 14, 2018
- 1 min read

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba Mfaransa, Pierre Lechantre jana amebwaga manyanga Rasmi kukinoa kikosi cha mabingwa wa Ligi kuu Bara Simba na kudaiwa kuondoka nchini baada ya Mkataba wake kufikia kikomo.
Lechantre alivaaa viatu vilivyo achwa na Mcameroon Joseph Marious Omog ambaye aliondoka Simba kwa kuto kuonesha kiwango kizuri cha kukinoa kikosi hicho
Kocha huyo alisaini mkataba wa miezi sita pekee ambayo imemalizika mwezi huu
Ujio wa Lechantre Simba umekuwa wa mafanikio japo kwa kipindi cha muda mfupi kwani kwa kushirikiana na kocha masaidizi Masoud Djuma ameweza kutwaa kikombe cha Ligi ku bara kwa Simba baada ya kukaa kwa kipindi cha zaidi ya Misimu mitatu bila kuchukua Kocha Msaidizi, Masoud Djuma amebaki na kikosi kwa sasa huku ikielezwa kuwa Suleiman Matola anaweza akaondoka Lipuli kuja kusaidiana na Djuma ambaye inaelezwa inawezekana akapewa Ukocha Mkuu.
Commentaires