top of page

FIFA YAONGEZA DAU A MSHINDI WA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU.

  • khalidi
  • May 9, 2018
  • 1 min read

Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limetangaza zawadi kwa washindi watakao shika nafasi sita za juu katika michuano ya Kombe la dunia mwaka 2018 yatakayofanyika nchini Russia

Aidha FiFA imeboresha na kuongeza zawadi za washindi kulinganisha na zile zilizotolewa katika mashindano ya mwaka 2014 yaliyofanyika nchini Brazil huku zawadi ya mshindi akiongezewa kitita cha Dola 3 million,

Katika fainali za mwaka 2014 mshindi wa kwanza ambaye alikuwa ni Jerumani aliibuka na kitita cha dola milion 35, huku mshindi aliyeshika nafasi ya pili Argentina alipata kitika cha Dola milioni 25 ,

Nafasi ya Tatu aliondoka na kitita cha Dola Milioni 20 kwa timu zilizoingia katika hatua ya makundi waliibuka na kitita cha million 8

FIFA imeboresha zaidi zawadi wakati msimu huu mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Dola Milioni 38 ongezeko la Dolla 3 millioni

Mshindi wa pili ataondoka na kitita cha Dola Million 28 ongezeko la Dola Million 3 kutoka Dola milioni 25

Mshindi wa Tatu atapata Dola Million 24 na mshindi wa Nne atapata Dolla Milioni 20 wote kwa ongezeko la Dola Milioni 2

Kwa timu zitakazo ingia katika hatua ya robo fainali zitaondoka na Dolla Million 16, hatua ya 16 bora wataondoka na Millioni 16 wakati maandalizi ni Dola Millioni 1.5 na makundi ni Dola Milioni 8.

コメント


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page