top of page

LISSU AANZA KUTEMBEA MWANYEWE

  • Fahari News
  • Jan 19, 2018
  • 1 min read

Afya ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji, inazidi kuimalika na sasa anafanya mambo mengi mwenyewe ikiwamo kwenda kuoga na kutembea kwa kutumia magongo.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), alipelekwa Ubelgiji Januari 7, mwaka huu, akitokea Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu tangu Septemba 7, mwaka jana.

Mbunge huyo aliumia vibaya baada ya kushambuliwa kwa risasi 32 na watu wasiojulikana nyumbani kwake mjini Dodoma Septemba 7, mwaka jana, tano kati ya hizo zilimpata katika maeneo mbalimbali ya mwili.

Vinceti Mghwai, ambaye ni mdogo wa Lissu, alisema kwa njia ya simu jana kuwa Lissu ameanza kutembea mwenyewe kwa kutumia magongo na kujipatia huduma mbalimbali ikiwemo kwenda kuoga bila msaada wa mtu mwingine.

“Tunamshukuru mungu sana, Lissu anaendelea vinzuri… tangu ameanza kupatiwa matibabu na mazoezi ya viungo tunaona mabadiliko makubwa mno,” alisema na kueleza zaidi:

“Maendeleo ni makubwa sana, kunavitu alikuwa hawezi kuvifanya lakini sasa hivi anatembea na magongo mwenyewe kwa kukanyagia mguu chini.

Anakula mwenyewe, “Tunaamini atatengamaa mapema zaidi, (na) haya kwetu ni maendeleo makubwa.

Mghwai alisema Lissu anapata muda mwingi wa kupumzika na huenda hivo ndiyo ikawa sababu kubwa ya yeye kuendelea kupona haraka kutokana na kupatiwa matibabu na bila usumbufu wowote.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page