top of page

AFYA PACHA WALIOUNGANA YAIMARIKA, WATOLEWA ICU

  • Fahari News
  • Feb 14, 2018
  • 1 min read

Dar es salaam. Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCA), Profesa Mohamed Jnabi amesema afya za pacha walioungana Maria na Consolata zinaendelea kutengemaa.

Profesa Janabi alisema pacha waliokuwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU) walishatolewa na wanaendelea vizuri na matibabu yao. Maria na Consolata walilazwa katika taasisi hiyo Januari 2 baada ya kupewa rufaa Mkoa wa Iringa waliofikishwa wakisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Tayari Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa wamefika Hospitalini hapo kuwajulia hali pacha hao wanaotibiwa chini ya jopo la madaktari bingwa sita wanaoongozwa na Profesa Janabi.

Pacha ni hao ni kati ya walemavu waliofanikiwa kuonyesha uwezo wao kielimu tangu walipohitimu na kufauru darasa la saba mwaka 2010 katika shule ya msingi Ikonda wilayani Makete, baadaye kidato cha nne katika sekondari ya udizungwa wilayani kilolo.

Mwaka jana pacha hao wanaosoma chuo kikuu cha Katoliki cha Ruaha (Rucu) waliofauru mitihani yao ya kidato cha sita iliyowezesha kuanza masomo ya ualimu chuoni hapo. Kwa sasa Maria na Consolata wanaelewa na serikali kwa kushirikiana na Rucu. Awali, walikuwa wakilelewa na Shirika la Masisita la Maria Consolata.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page