UOKOAJI KWA HELKOPITA M’KILIMANJARO WAANZA
- Fahari News
- Apr 3, 2018
- 1 min read

Kampuni ya kwanza ya kipekee ya utafutaji na uokoaji wa wapanda milima kwa kutumia helkopita nchini (Kilimanjaro SAR), imeanza kutekeleza rasmi shughuli zake za uokoaji katika Mlima Kilimanjaro na Mlima Meru.
Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Ivan Braun, alisema ujio wa huduma hiyo unaleta usalama kwa kuanzisha kliniki ya kwanza Afrika maalumu kwa matibabu ya magonjwa yatokanayo na mlima.
“Kilimanjaro SAR inabeba rekodi ya kwanza duniani ya kampuni za uokoaji, kwa kuwa teyari ndani ya dakika tano baada ya kupokea simu ya hitaji la msaada, Kampuni hii itatoa huduma kamili ya uokoaji wa dharura kwa wapanda mlima katika hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro na Mlima Meru, mkoani Arusha,” alisema Braun.
Kampuni ya utafutaji na uokoaji kwa kutumia helkopita iliyoanzishwa mwaka 2016 nchini Tanzania na mtaalamu wa zamani wa kupanda milima kutokea nchini Denmark, Ivan Braun, lengo kuifanya Kilimanjaro kuwa sehemu salama zaidi ya utalii Afrika.
Kilimanjaro SAR imewekeza zaidi a Dola za Marekani milioni tatu kwaajili ya kuazisha kliniki hiyo ya tiba Afrika itakayosaidia watalii wanaopata ajali na kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa katika hifadhi hizo.
Comments