KIGWANGALLA ATENGUA UTEUZI BODI YA NGORONGORO
- Khalidi
- Dec 20, 2017
- 1 min read

Waziri wa Maliasili na Utalii, DK. Hamisi akaigwangalla, ametengua uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambao wamehudumu kwa siku 14 tangu kuteuliwa kwao.
Utenguzi huo unakuja ikiwa ni siku chache tu tangu Rais DK. John Magufuli alipomteua Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Profesa Abiud Kaswamila, Decemba mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na vyombo vya habari na katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi, haikuelezwa sababu ya kumtengua kwa uteuzi wa wajumbe
hao. “Uteuzi wa wajumbe wapya wa bodi hiyo utafanyika ndani ya siku chache zijazo, tunawashukuru wajumbe hao kwa kuhudumu katika bodi kwa kipindi hicho,” alisema Meja Jenerali Milanzi.
Comentários