VYOMBO VYA HABARI VYA TAJWA KUSHUHSA UTALII MAPANGO YA AMBONI
- Khalidi
- Jan 8, 2018
- 1 min read

Mhifadhi mkuu wa kituo cha mapango ya Amboni Jumanne Mabula amesema idadi ya watalii wanaotembelea mapango hayo imeshuka na kusaabisha kuporomoka kwa mapato kutokana na athari za taarifa zilizokuwa zikiripotiwa kwenye vyombo vya habari juu ya uwapo wa wahalifu waliojificha kwenye mapango hayo
Amesema wahalifu walijificha katika mapango ya Amboni kata ya Mzizima zaidi ya Kilometa 20 kutoka kwenye mapango yanayotumika kwa shughuli za utali lakini ripoti za vyombo vya habari zilionesha kwamba walijificha sehemu ambazo utalii umekuwa ukifanyika
Aliongeza kuwa tangu kuripotiwa kwa taarifa hiyo idadi ya watalii ilishuka na kusababisha kuporomoka kwa mapato
Alibainisha katka kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 idadi ya wataliii waliotembelea mapango hayo ilikuwa ni 27,000 na mapato ta yaliyotokana na idadi hiyo yalikuwa ni zaidi ya Sh milioni 26
Mabula alisema kuwa baada ya kuripotiwa kwa taarifa hizo mwaka wa fedha wa 2015/2016 idadi ya watalii ilishuka hadi kufikkia wastani wa 8,000 na mapato yalikuwa shilini milioni 16
Hata hivyo mhifadhi huyo alisema hali ilianza kuimarika mwaka jana watalii waliyatembelea mapango hayo tofauti na kipndi cha nyuma
Commentaires