top of page

MUME NA MKE WAUAWA KIKATILI, WATOTO MAJERUHI

  • Khalidi
  • Dec 14, 2017
  • 1 min read

Mume na mke wameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga usiku Mkoani Singida, huku watoto wao wawili wakijeruhiwa vibaya kutokana na ugomvi wa familia mbili zikigombea mashine ya kusukuma maji kwaajili ya kilimo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, aliwataja majeruhi hao ni Kija Kitundu Zephania (53) na Mwajuma Ramadhan Yindi (59), wakazi wa kijiji cha Ishenga Wilaya ya Mkalama.

Kamanda Mgiligimba alisema tukio hilo lilitokea saa sita usiku wa Desemba 10,mwaka huu nyumbani kwa wanafamilia hao, huku watoto Namagalu Kija (12) na Ramadhan Kija (14) wakinusulika kifo kwa kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao.

Alisema uchunguzi wa polisi umebaini chanzo cha vifo hivyo ni chuki iliyosababishwa na mashine aina ya King Max namba GX 200, iliyonunuliwa mwaka 2015 na Juma Shilla (43) , lakini wanandoa waliouawa wakadai ni maji yao.

Alifafanua katika upelelezi huo ulibaini lengo la kununuliwa kwa mashine hiyo ni kutumiwa kwenye kilimo cha kiangazi na familia hizo, lakini marehemu hao walikataa na hapo ndipo ugomvi na chuki vilipoanzia.

Magiligimba alisema wavamizi waliingia katika nyumba hiyo usiku kwa kuruka na kupitia kwenye paa ambalo lilikuwa wazi bila kuezekwa kwa bati kwa kutumia ngzi kasha kutumbukia ndani.

Kutokana na mauaji hayo, walisema watu 10 wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi akiwamo Juma Shilla, Jumapili Shilla (32), Jumatatu Shilla(29), Shilla Mzimbu (75) na Kasala Lugoye (20).

Wengine ni Shilla Joseph (18), Gabriel Shalua (45), Johari Pyuza (20), Fanuel Pendael (34) na petro Joseph (23), wote wakazi wa Kijiji cha Ishenga Tarafa ya Kinyangiri na taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page