MAFUNGU MALIPO KIFO BIL. MSUYA YALIVYOKUWA
- Fahari News
- May 11, 2018
- 2 min read

Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi imeelezwa kwamba mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite ‘Bilionea’asto Msuya (43), aliwalipa wahusika wa mauaji hayo sh. Milioni 10 muda mfupi baada ya kutoka eneo la tukio.
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni Sharif Athuman (35) madini ya Tanzanite na mchimbaji mdogo katika migodi ya Mirerani iliyopo wilayani ya Simanjiro, mkoa wa manyara manayemiliki migodi mitatu ya madini mitatu ya madini hayo eneo la kitalu ‘B’
Mahakama hiyo ilielezwa hayo jana na shahidi wa 27 wa upande wa Jamhuri, Mkaguzi wa polisi Damian Chilumba, kutoka Ofisi ya Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai, kanda Maalumu ya Dar es salaam.
Mkaguzi Chilumba alidai hayo baada ya Jaji Salma Maghimbi kuruhusu kusomwa maelezo ya onyo ya Athuman ambayo yanadaiwa ni ya kukiri kosa.
Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi 22, Agosti 7, mwaka 2013, majiraa ya saa 6:30 mchana katika eneo la Mijohoroni, kando ya barabara kuu ya Arusha- Moshi, karibu na Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Akisoma maelezo hayo, shahidi huyo alidai mshtakiwa wa kwanza alimweleza kwamba aliwalipa watuhumiwa wa mauaji hayo sh milioni 10 muda mfupi tu baada ya kutekeleza mauaji ya Msuya na kwamba awali wakati wakisuka mipango hiyo alikuwa amewalipa sh. Milioni sita.
Aidha, mkaguzi Chilumba alidai mshtakiwa huyo wa kwanza alimweleza kwamba aliwaambia watuhumiwa wa mauaji hayo kwamba kiasi kilichobakia, angewalipa baada ya kukutana na mfanyabiashara mwenzake wa madini.
Mshtakiwa huyo anadaiwa pia aliwaeleza watuhumiwa wa mauji hayo kwamba baada ya kumuua Msuya wasichukue kitu chochote.
Katika maelezo hayo, mahakama hiyo ilielezwa kuwa mshtakiwa wa kwanza alibeba bunduki aina ya SMG kutoka nyumbani kwake eneo la kimandolu mkoani Arusha na kwenda hadi KIA na kisha kumkabidhi silaha hiyo mshtakiwa wa tano, Karim Kihundwa ambaye siku ya tukio hilo alikuwa amevaa tisheti nyeupe ndani na koti la kaki.
Shahidi huyo aliendelea kudai kwamba mshtakiwa wa kwanza alimweleza kwamba yeye anamiliki migodi mitatu ya madini ya Tanzanite iliyopo kitalu ‘B’ na anamiliki pia nyumba ya kulala wageni ya Shamoo Guest House, Super Market.
Comments