APATA FAHAMU KABLA YA MADAKTARI KUAMUA KUMUUA
- khalidi
- May 9, 2018
- 1 min read

Mvulana wa miaka 13 katika jimbo la Alabama nchini Marekani alipata fahamu baada ya wazazi wake kutia saini stakhabadhi za kukatisaha maisha yake ili kufadhili viungo vyake vya mwili.
Trenton McKinley aliugua tatizo la ubongo alipoanguka katika trela ya gari ambayo ilimuangukia katika kichwa chake na fuvu la kijana huyo lilivunjika mara saba katika ajali hiyo mjini Alabama mnamo mwezi Machi.
Madaktari waliambia wazazi wake kwamba hawezi kupona na kwamba viungo vyake vilikuwa vikifanana na vile vya watoto wengine watano ambao walihitaji kupandikizwa.
Bi Reindl alikubali kutia saini stakhabadhi za kufadhili viungo vya mwili, Siku iliofuata alitarajiwa kufanyiwa kipimo cha mwisho cha ubongo wake ili kumsaidia kufa,

Siku moja kabla ya maisha yake kuondolewa , Trenton alionyesha ishara za kupona.
Hali hiyo ilipelekea madakatari kuahirisha zoezi la kutoa uhai wake na Trenton sasa anaendelea kupona polepole .
"Nilijigonga kichwa na sakafu na baadaye trela ikaniangukia kichwani. Baada ya hilo sikumbuki chochote'' , alisema.
Bado ana maumivi na ameshtuka. Na atahitaji upausuaji ili kuunganisha fuvu lake la kichwa.
''Amekuwa akitembea na kuzungumza hata kusoma na kufanya hesabati'' , bi Reindl alisema akitarajia kuwa miujiza.
Trenton mwenyewe alidai kuwa alidhania kwamba alikuwa mbinguni wakati alipokosa fahamu.
''Nilikuwa katika uwanja ulio wazi nikitembea'' , alisema kijana huyo.
''Hakuna maelezo isipokuwa Mungu pekee''.
Familia imeanza kuchangisha fedha katika mtandao wa Facebook ili kumsaidia kimatibabu
Comments