VIGOGO BENKI YA UMMA MATATANI
- Fahari News
- Apr 16, 2018
- 3 min read

Waziri wa Kilimo DK Charles Tizeba leo anatarajiwa kujibu hoja zilizoelekezwa kwa wizara yake na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kubwa ikiwa hatua ambazo serikali inachukua dhidi ya ‘Vigogo’ waliobainika kutumia vibaya mabilioni ya shilingi kwenye Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).
Tangu kuwasilishwa Bungeni mjini hapa kwa ripoti ya CAG kwa mwaka 2016/17, mawaziri wamekuwa wakijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa, na leo ni zamu ya Wizara ya Kilimo inayoongozwa na DK. Tizeba na wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyochini ya Luhaga Mpina.
Katika ripoti yake kuhusu mashirika ya umma. CAG Prof. Mussa Juma Assad, anabainisha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha za TADB.
Anaeleza kuwa ukaguzi wake katika benki hiyo umebaini kuwapo mchezo mchafu wa fedha zake kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalum (Fixed Deposit Account) badala ya kusaidia sekta ya kilimo, ambalo ndiyo lengo la kuanzishwa kwake.
Prof. Assad anaeleza katika ripoti yake kuwa amebaini kiasi cha sh bilioni 54.7, ikiwa ni asilimia 91 ya mtaji wa benki hiyo, kiliwekwa kwenye akaunti ya muda maalum.
Anasema TADB ilianzishwa Septemba 2011 chini ya sheria ya Kampuni ya mwaka 2002, jukumu lake kubwa likiwa ni kusaidia maendeleo ya sekta ya kilimo na haipaswi kufanya biashara.
“Benki iliazishwa kwa lengo la kutoa huduma za muda mfupi, wa kati ya mrefu kwa sekta ya kilimo, huduma zaa kifedha kusaidia ukuaji wa shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji na kuwezesha tafiti za sekta hiyo,” anaeleza Prof. Assad katika ripoti yake hiyo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka wawekezaji wa viwanda vya nyama ya punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao kutoka sh 200,000 za sasa.
Endapo bei hiyo itapanda, alisema waziri huyo, kutakuwa na udhibiti wa utoroshaji wa mifugo hiyo kwenda nje ya nchi.
Inakadiliwa kuwa zaidi ya punda 10,000 hutoroshwa mipakani kwa siku kwenda nje ya nchi wanakonunuliwa kwa bei ya juu.
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda cha nyama ya punda cha Hua Cheng nje kidogo ya mji wa Dodoma jana na ambacho alikifungua hivi karibuni, waziri Mpina alisema sh 200,0000 haziendani na gharama halisi ya ufugaji wa punda. Alisema kwa kuwa kiasi hicho ni kidogo, ndiyo maana wafugaji hutorosha mifugo hiyo na kukosesha taifa mapato mengi.
Mpina alisema ili punda aweze kufikia hatua ya kuchinjwa huchukua kiasi cha miaka miwili hivyo gharama zake za ufugaji kuwa juu ukilinganisha na kiasi kinachotolewa na wenye viwanda vya nyama ya punda nchini.
Utoroshaji wa mifugo unaokadiliwa kufikia 1,614,035 kwa mwaka unaofanyika kwenye mipaka ya nchi unakadiriwa kutia hasara y ash bilioni 32.28 kama ushuru na takribani sh bilioni 24.21 za kodi ya mapato ambayo ingepatikana katika nyama ambayo ingeuzwa nchini.
Wakati huohuo waziri wa mifugo, na Uvuvi, Luhaga Mpina ameunda tume ya wataalam kutoka wizarani kufanya tathimini kama kiwanda hicho kimetimiza mashariti yote yaliyotolewa na serikali baada ya kukifungulia adhabu Februari mosi, mwaka huu.
Alisema ikibainika kama hakijakidhi masharti yaliyotolewa mwaka jana, kitachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kukifungi kufanya kazi.
Aliyataja baadhi ya mashariti aliyoyatoa wakati wa kukifungia kiwanda hicho Julai 2017 kuwa ni pamoja na kuwa na ranchi ya kuunda na kuingia mikataba na vikundi vya wafugaji wa punda.
Aidha, kiwanda cha Hua Cheng kilitakiwa kilitakiwa kuwa na punda wasiopungua 300 katika eneo la kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa ili kuhakikisha kwamba mifugo wanaangaliwa kwa wiki mbili kabla ya kuchinjwa ili wawe katika ubora wa kimataifa.
Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho, Xun Long Go alimshukuru Waziri Mpina kwa kuondoa adhabu na kwamba hadi sasa kimezarisha na kuuza tani 224 za nyama ya punda kwenda China na Vietnam.
Alisema pia tani 52 za ngozi ya punda ilizalishwa na kuuzwa katika miezi miwili iliyopita.
Alisema kiwanda hicho kimeajili Watanzania 55 ambapo hadi sasa kina punda 88 katika maeneo ya Chalinze mkoani pwani na Zuzzu mkoani Dodoma.
Tanzania ina viwanda wiwili vya kuchinja na kuuza nyama ya punda. Kingine ni Fang Hua kilichopo Shinyanga ambavyo vyote vimepewa kibali cha kuchinja wanyama 20 kwa siku kila kimoja.
Kommentit