top of page

PASPOTI YA KAKOBE YAZUIWA UHAMIAJI

  • Fahari News
  • Apr 10, 2018
  • 1 min read

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam, inashikiria hati ya kusafiria ya Askofu Mkuu wa Kanisa l Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe, kuchunguza uraia wake.

Hati ya kiongozi huyo wa kiroho alishikiriwa jana alipokwenda kuitikia wito wa idara hiyo.

Askofu Kakobe aliwasili katika ofisi za idara hiyo saa 4:52 asubuhi akiongozana na wasaidizi wake wanne na alihojiwa kwa takribani saa tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahojiano hayo, Askofu Kakobe alisema yeye ni raia halali wa Tanzania.

“Anayesema mimi si raia wa Tanzania aniambie ni raia wan chi gani.” Alisema.

Alisema uhamiaji wanaweza kuwa na nia njema lakini alihoji kwanini kwa sasa wanahojiwa watu Fulani kutoka Kigoma. “Kwanini sasa, wanawahoji watu wa aina Fulani kwa kutoka eneo Fulani la Kigoma. Mbona hatujasikia kutoka Dodoma, Kaskazini wakihojiwa?

“Mimi ni mtanzania na kama kuna mtu anasema si raia, basi aniambie mimi ni raia wan chi gani,” alisema Askofu Kakobe.

Alisema katika mahojiano hayo, ametakiwa kuacha hati yake ya kusafiria ili iweze kuwasaidia kupata taarifa zake muhimu.

“Hiki wanachokifanya kinatia shaka. Biblia inasema muovu anakimbia hata kabla ya kufuatwa na mtu ila mwenye haki ni jasili kama simba.

“Lakini wamesema ni kitu ambacho kitachukua siku moja au mbili kwasababu wanataka kuangalia kwenye mafaili ili kupata taarifa za hizo (affidavit) zinazotakiwa,” alisema.

Kuhusu kuchunguzwa uraia wake Askofu Kakobe alisema si jambo la ajabu kutokana na sheria kuruhusu idara hiyo kumuhoji mtu yeyote ila wasiwasi wake ni muda ambao suala hilo linafanyika.

Alisema kabla ya jana kuhojiwa, maofisa wa idara hiyo wamekuwa wakienda nyumbani kwao kijiji cha Mbizi, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kumfuatilia nay eye amekuwa akipata taarifa hizo kwa ndugu zake.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page