JPM KUHUTUBIA BUNGE LA EALA
- Fahari News
- Apr 10, 2018
- 1 min read

Rais John Magufuli anatarajia kuhutubia Bunge la Afrika Mashariki (Eala) katika mkutano wake wanne ulioanza jana mjini Dodoma, ikiwa ni mara ya kwanza vikao vya bunge hilo kufanyika mjini humo.
Taarifa ya Eala kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi habari habari mwandamizi, Bodi Odiko alisema mkutano huo umeanza jana na utamalizika Aprili 28, siku ambayo Rais Magufuli atahutubia.
Spika wa Bunge hilo, Martin Ngoga ataongoza Mkutano huo wa wiki tatu ambao utajadili miswada na maazimio mbalimbali.
“Kwa sasa ipo miswada miwili itakayojadiliwa kwa kina inayohusu itifaki ya sarafu moja; muswada wa taasisi ya fedha na muswada wa takwimu yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2017,” alisema Odiko.
Alisema miswada hiyo iliwasilishwa katika bunge hilo la mwanyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Eac, DK Kirunda Kivenjija na ilishasomwa kwa mara ya kwanza katika mkutanio wa pili uliofanyika Januari jijini Kampala, Uganda.
Comentários