top of page

CHINA KUJENGA VIWANDA 200 NCHINI, KUAJIRI LAKI 2

  • Fahari News
  • Apr 10, 2018
  • 2 min read

China katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.

Kwa sasa uwekezaji wa china nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja 350,000.

Taarifa hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, katika hafla ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered.

Waziri Mwijage alisema amefurahishwa na kauli iliyotolewa na Benki hiyo kwamba inawekeza Dola za Marekani billion 20 sawa na fedha za Kitanzania trioni 40 katika kampeni ya china ya uwezeshaji mitaji na biashara kutoka Asia kwenda nchi nyingine za dunia.

Kampeni hiyo inayoitwa One Belt One Road, inagusa nchi 65, Tanzania ikiwamo.

Aliisifu Benki hiyo kwa kuandaa hafla hiyo kwa wateja wake wa china ikiwa ni sehemu moja ya kutangaza kampeni hiyo ya china na kuwafanya wananchi wengi kuelewa fulsa zinazoambatana nazo.

Alisema kwa sasa Tanzania inapigana kuingia katika uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda na kampeni ya China inakwenda sawa na mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliokazania uwekezaji katika viwanda.

Alisema kwa sasa serikali inaweka vyema mazingira ya uwekezaji na ikiwa na uchumi unaokuwa kwa kasi wa asilimia 6 hadi 7, juhudi za benki hiyo za kuonesha fursa za uwekezaji na uendeshaji wa uchumi zinakaribishwa na serikali ya Tanzania.

Katika hotuba hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi, alisema kwamba mpango huo wa China unaozungumzia uwekezaji wa mitaji na biashara kutoka Asia kwenda nchi nyingine.

Alisema pia ni kichocheo cha kukua kwa uchumi duniani na kutaka Watanzania kushiriki kikamilifu.

Awali ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo nchini Tanzania, Sanjay Rughani, alisema Benki ya Standard Chartered duniani inawekeza katika Belt and Roads Initiative kiasi cha dola bilioni 20 sawa n ash trioni 44.8 za kitanzania kuwezesha miradi mbalimbali kwenye kampeni hiyo ya China.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page