top of page

MIGUNA MIGUNA ATUA CANADA, AAHIDI KURUDI KENYA

  • Writer: Admin
    Admin
  • Apr 3, 2018
  • 1 min read

Mwanasheria aliyefurushwa kutoka Kenya, DK. Miguna Miguna ametua nchini hapa baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai, ambako alitumia siku nne.

Mmoja wa wanasheria wake, Nelson Havi, alisema jana DK. Miguna aliondoka Dubai kwa hiari kwa usaidizi wa ubalozi wa Canada anayehudumu katika muungano wa Falme za Kiarabu (UAE).

“Alisafiri na kuwasili Torondo, Canada. Atafanyiwa uchunguzi wa kupata matibabu kutokana na kemikali alizotumia kumlaza usingizi kuwa na sumu. Atarudi Kenya baada ya matibabu” Hivi alituma ujumbe katika akaunti yake, ya Twitter.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kinachofahamu suala hilo, ,DK Miguna aliondoka Dubai na shirika la ndege Canada baada ya kuonyesha hati ya kusafiria ya Canada, ambayo ilidaiwa kuibiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyetta (JKIA) Mjini Nairobi.

“Mamlaka za UAE zimeanza uchunguzi wa namna alivyoipata hati yake ya kusafiria baada ya kushindwa kuonyesha kwa mamlaka wakati akiondoka kutoka Kenya na kuwasili Dubai.

“Kenya pia inataka kuchunguza namna alivyoipata hati yake ya kusafiria baada ya kuzituhumu mamlaka za Kenya kumwibia wakati wa mvutano JKIA,” kilisema chanzo hicho kilichozungumza kwa masharti ya kutotajwa kwa sababu hakina mamlaka ya kuzungumza kwa vyombo vya habari.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page