BOT YATOA AGIZO KWA BENKI
- Fahari News
- Mar 26, 2018
- 2 min read

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), DK. Bernad Kibesse, ameyataka mabenki yote nchini kupunguza riba ili kuwapa unafuu wa mikopo wafanyabiashara.
Pia alisema tayari Benki Kuu imeshapunguza riba kwa mabenki ili ziweze kukopa na kujiendeleza kwa mitaji itakayowapa unafuu wa kuwakopesha wananchi.
Hayo yaliyosemwa mwishoni mwa wiki Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Benki ya Standard iliyolenga kuangalia mchango wake katika masuala ya jamii na uchumi Afrika Mashariki.
Alisema pamoja na jitiada nyingi ambazo Benki Kuu imefanya nia ni kuona mabenki hayo yanaweza kukopesha wananchi kwa unafuu na kwamba tayari wameanza kuona mabadiliko ya mabenki kuwa na riba ndogo.
Dk. Kibesse aliipongeza ripoti yao kwa kuonyesha inachangia asilimia moja katika ukuaji wa pato la Taifa na ukuaji wa pato la Taifa na ukuaji wa uchumi pia.
“Sisi tunafurahia mchango wa benki hii unaonekana kwa maana haifanyi kazi tu Dar es salaam, inajikita katika mikoa mingine pia, hivyo hakuna budi mabenki mengine yakaiga mfano huo,” alisema DK. Kibesse.
Naye mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante Gabriel, alisema taasisi za fedha zinatakiwa kuiga mfano na kuangalia ni jinsi gani zinaweza kutoa huduma wezeshi kwa wafanyabiashara kwa riba ndogo.
Aliishauri Benki ya Standard Charted ba mabenki mengine kutoa mikopo isiyo na riba kwa vijana na hasa katika maeneo ya vijijini.
“Wizara yetu itaendelea kushirikiana na mabenki, wafanyabiashara pia ili kuwa na uchumi wa viwanda na mabenki watoe ushirikiano ili tuweze kuwaunganisha na taasisi zilizo chini yetu kama vile Tan-Trade, Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido),” alisema Profesa Gabriel.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Ruth Zaipuna, alisema benki imejizatiti kuhudumia Watanzajia , lengo ni kusukuma maendeleo ya Tanzania na Afrika Mashariki. Alisema katika kumsapoti Rais DK. John Magufuli ndio maana wamechangia kutoa ajira kwa watu zaidi ya laki mbili ambazo ni za moja kwa moja na wale walioajiliwa kwa wengine.
Comments