top of page

KESI MKURUGENZI TPDC KALENDA

  • Fahari News
  • Mar 21, 2018
  • 1 min read

Kesi inayowakabili

, james mataragio na wenzake wanne ya matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia dola za marekani 3,238,9836.50 imepigwa kalenda hadi april 18 mwaka huu baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Mbali na mataragio washtakiwa wengine ni meneja utafutaji, George semi, mkuu wa manunuzi na utawala, wellington Hudson, mkurugenzi wa idara ya fedha, Kelvin komba na kaimu mkurugenzi mipango mkakati , Edwin riwa.

kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya vigogo hao kuwasilisha hati zao za kusafiria mbele ya hakimu mkazi mkuu, wilbard mashauri.

Wakili wa serikali, Emmanuel Jacob, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kwamba ilipangwa kwa ajili ya kwashtakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria.

Ujumaa washtakiwa hao walisomewa mashataka yao kwamba kati ya april 8,2015 na juni 3,2016 washtakiwa wakiwa wtumishi wa umma na waajiriwa wa TPDC wakati wakitekeleza majukumu yao kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kubadilisha na kuptisha bajeti na mpango wa mwaka 2015/16 wa manunuzi kwa lengo la kujipatia manufa ayasiyo halali ya dola za marekani 3,238,986.50

Ilidaiwa kuwa washtakiwa waliingiza kifaa cha kupima kiitwacho ‘BellGeospace’ katika ziwa Tanganyika bila kupata Baraka za bodi ya wakurugenzi TPDC, kitendo ambacho walikiuka kifungu cha 49 (2) , cha sheria ya manunuzi ya umma ya 2011. Washtakiwa walikana mashtaka yao.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page