WAWILI WAFARIKI DUNIA MTO RUBANA
- Fahari News
- Mar 20, 2018
- 1 min read

WAKAZI wa kijiji cha Makundusi kata ya Natta wilayani Serengeti wamefariki dunia na wengine wawili wamenusurika kifo baada ya kusombwa na maji yam to rubana imefahamika.
Mto huo ulikuwa umefurika kutokana na mvua inayoendelea kunyesha wilayani hapa.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi asubuhi.
Alisema watu hao walikutwa na mkasa hyo walipokuwa wakivuka mto huo kwenda kuchunga ng’ombe katika pori la akiba la Grumeti.
Babu aliwataja waliofariki dunia ni chacha mwita(20) na mwita kimwencha (38) na miili yao imepatikana na kuokolewa.
Walionusurika na kuokolewa na wananchi ni Nsamaki mzuki na sagana ikamura, alisema.
Babu alisema mvua inayoendelea kunyesha kwa wingi wilayani hapa imesababisha mito kujaa maji.
“ jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wmefika eneo la tukio kujiridhisha na mazingira yaliyosabbisha vifo vya watu hao wwili ili kuruhusu taratibu za mazishi kuendelea “ alisema babu.
Alisema mto rubana hupokea maji mengi kutoka mito midogo nyanda za juu a wilaya ya Serengeti hivyo husababisha kufurika wakati wa mvua ya masika.
Mto huo unapita katikati ya hifadhi ya taifa ya Serengeti maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakichunga mifugo yao .
Comments