top of page

MTULIA AWATANGAZIA NEEMA WAKAZI WA MABONDENI.

  • Fahari News
  • Mar 20, 2018
  • 1 min read

MBUNGE Mteule wa kinondoni , mauled mtulia (CCM) amesema yupo katika mchakato wa makubaliano na serikali ya kuwapatia viwanja wakati wa mabondeni katika jimbo lake ambao nyumba zao ziko kwenye orodha ya kubomolewa.

Mtulia aliyasema hayo jana katika mahojiano maalum na MTANZANIA yaliyofanyika dare s salaam .

Alisema atawapigania wakazi wa jimbo lake mpaka watakapopata haki yao na kusistiza kuwa walikuwa kwenye oridha ya kesi ya kupinga kubomolewa nyumba zao watapewa viwanja katika maeneo mengine.

“wakazi wa mabondeni waliniuma sana kwani hata mimi niliishi mabondeni zamani lakini nilipokuwa nahangaika nao na hata kufungua kesi ya zuio mahakamani na madai ya fidia sikuwa katika upande sahihi.

“Na hiyo ndio sababu ilinifanya niende CCM. Nilitaka niwe karibu na serikali ili niwatetee wkazi wa mabondeni kwa sababu mimi kuwa mbunge wa upinzani nisingeweza kuwatetea. Na katika hili nitahakikisha nashirikiana na serikali ili kufikia lengo hili” alisema mtulia.

Aidha alisema akishaapishwa atafanya kikao na madiwani wa vyama vya chadema, CUF, na CCM na ajenda yake itakuwa kupanga mikakati ya kuendelaza jimbo.

Mtulia alisema uchaguzi umeshakwisha na haamini ktika kuendeleza chuki hivyo atawaita madiwani wote kupanga jinsi ya kuendelez ajimbo. Alisema tama yake ni madiwani wote kuungana lakini ikitokea baadhi wataamua kujiweka pembani watakuwa kikwazo cha kutafuta maendeleo ya wana kinondoni.

“mimi mbunge wao nawabembeleza sana tuwe pamoja madiwani wanguf 10 nawaomba tuwe pamoja bila kujali itikadi za vyama. Katika jimbo langu kuwa madiwani watatu wa CUF watau wa Chadema , hao sita kama watajitenga maendeleo yatachelewa kinondoni.

Commentaires


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page