MWALIMU MBARONI AKITUHUMIWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
- Fahari News
- Mar 15, 2018
- 1 min read

Mwalimu wa shule ya sekondari Adili ya jijini hapa, Joel Mbaga (27), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake mwenye miaka 13.
Mtuhumiwa alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda jana. Mwendesha mashtaka wa serikali, Naomi Mollel, alidai mahakamani hapo kuwa Joel alitenda kosa hilo kati ya Septemba na Oktoba mwaka 2017. Mama wa mtoto huyo, Agnes John(41), ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, alisema alibaini mtoto wake amefanyiwa kitendo hicho baada ya kugoma kwenda shule. “Ilikuwa Oktoba 30 mwaka jana, mtoto alirudi nyimbani na kugoma kwenda shule na baada ya kumhoji, alisema mwalimu alikuwa akimlawiti,” alidai Agnes. Alidai baada ya kumchunguza, alimkuta na michubuko sehemu za siri na ndipo alikwenda kutoa taarifa polisi na baadaye kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Agnes alidai baada ya kumfikisha Hospitali, alilazwa siku mbili na alibainika kuingiliwa sehemu za siri. Hata hivyo mwalimu Mbaga alikana tuhuma hizo. Hakimu Kisinda aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 3, mwaka huu ambapo shahidi wa tatu ambaye ni daktari aliyemchunguza mwanafunzi huyo alitoa ushahidi. Mwalimu huyo ataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Commentaires