top of page

DPP AKABIDHIWA JALADA LA KESI MAUAJI YA BODABODA BUGURUNI

  • Fahari News
  • Mar 14, 2018
  • 1 min read

Jalada la kesi ya mauaji ya waendesha bodaboda wawili eneo la Buguruni inayowakabili watu 20, lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwaajili ya uchunguzi.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 59 ya mwaka 2015, iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji ya Hamid Mwanangu na Jafari Hamisi.

Wakili wa serikali, Elia Athanas alieleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wakati kesi hiyo ilipokuwa kwaajili ya kutajwa.

wakili A thanas alidai kuwa ulelelezi wa shauri hilo, upo katika hatua za mwisho za kukamilika na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

“Washtakiwa wote wapo mbele ya Mahakama yako na jalada la kesi hili bado lipo kwa DPP, lakini upelelezi wa shauri hili upo katika hatua za mwisho za kukamilika, hivyo hivyo tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alidai wakili Athanas.

Awali, wakili wa utetezi, Alex Massaba alidai kuwa tangu washtakiwa hao wafunguliwe shtaka hilo, Desemba 4, 2015 hadi sasa upande wa mashtaka wamekuwa wakidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 20, itakapotajwa.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page