top of page

ASKARI MAGEREZA WASOTA RUMANDE

  • Fahari News
  • Mar 14, 2018
  • 1 min read

Askari magereza 11 Wilayani Korogwe mkoani Tanga wanadaiwa kumuua mwanakijiji, Aloys Makalla, wanaendelea kusota mahabusu, baada yaa kesi yao kuahirishwa.

Kesi hiyo iliahirishwa tena jana kwa mara ya nne na mahakama ya wilaya ya korogwe mkoani Tanga. Askari hao wanaohukumiwa kwa kumuua Makalla, mkazi wa kijiji cha kerenge, kata ya Kerenge, Wilayani Korogwe.

Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Albert Nyang’ali, ambaye alisoma shtaka hilo la mauaji kama mlinzi wa amani, alisema sababu ya kuendelea kutajwa shauri hilo bila kupangiwa kusikilizwa ni kutokana na baadhi ya vipengele kufanyiwa marekebisho.

Nyang’ali aliwataja askari hao ambao wapo mahabusu ya gereza la Wilaya ya Korogwe ni P 5377 Inspekta Makere, A 4921 RSM (Mkuu wa Nidhamu) Mokiwa Shadrack Lugendo, A, 7367 Sajenti Mussa Mdoe Seif, B 5919 Koplo Lazaro Stephen Nyota, B, 5486, Koplo Ramadhan Yusuph, B 7087 WDR Robert Alfred B, 7980 Fidirishi Cosmas.

Awali alidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja Januari 22, 2018 katika kijiji cha Kerenge wilayani Korogwe walimuua Aloyce Makalla maarufu kama Mapi.

Katika kesi hiyo namba 2P1 ya mwaka 2018, watuhumiwa wote walikana shtaka, lakini hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Shauri hilo limepangwa kutajwa tena Machi 26, mwaka huu. Hii ni mara ya nne kesi hiyo kutajwa huku, watuhumiwa wote wakirejeshwa rumande.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page