MRADI MWENDO KASI MBAGALA WAPIKWA
- Fahari News
- Mar 13, 2018
- 1 min read

Wakati abiria 200,000 wanaohudimiwa na Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) JIJINI Dar es salaam kila siku kwa sasa , awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi hayo inayohusisha barabara ya kwenda Mbagala imeanza kupikwa.
Teyari serikali imetangaza zabuni ya ujenzi waawamu hiyo ambapo waliovutiwa na zabuni hiyo wanatakiwa kuwa na dhamana isiyopungua sh 480 milioni na kuwasilisha maombi yao kipindi kisichozidi Aprili 10.
Kwa mujibu wa Tangazo la zabuni hiyo lilitolewa baada ya serikali kupata mkopo kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), mradi utahusisha ujenzi wa jingo la biashara (Mbagala Complex) litakalokuwa na karakana, maduka, ofisi za utawala, maliwato na kituo cha abiria.
Vilevile kutakuwa na vituo vinane vya abiria, kituo cha mafuta, kituo cha polisi, Vibanda vya ulinzi, uzio na maegesho ya magari.
Ndani ya siku 730 za utekelezaji wa mradi huo zikiwamo 56 za maandalizi, pia kutakuwa na ujenzi wa vituo Kariakoo, Mbagala Zakhem, Mtoni Kijichi, Mtoni na Chang’ombe.
Licha ya kutangazwa na AfDB, maombi yote ya mradi huo yanatakiwa kupelekwa makao makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ndani ya muda uliotolewa.
Mkurugenzi mtendaji wa Tanroads, Patrick Mfugale alisema wanasubiri kupokea maombi hayo kabla hawajatekeleza majukumu yao ya kumtafuta atakayeshinda na kumpa jukumu la kuutekeleza.
Ingawa zabuni hiyo ya kimataifa, waombaji ambao wanaweza kupata taarifa zaidi na kukagua nakala husika kutoka ofisi ya katibu mkuu wa ujenzi wanapaswa kutoka kwenye nchi wanachama wa AfDB pekee.
Kuazia siku ya mwisho ya kupokea maombi ya zabuni hiyo, tangazo linasema mapitio yatafanywa kwa siku 120 kabla ya kutangazwa kwa mshindi.
Commentaires