top of page

DC, DK NAGU WAPATANISHWA

  • Writer: Admin
    Admin
  • Mar 13, 2018
  • 2 min read

Hanang. Wagombanao ndiyo wapatanao, ndivyo unavyoweza kusema baada ya mkuu wa wilaya na Mbunge wa Hanang mkoani Manyara kupatanishwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa. Mkuu wa wilaya, Sarah Msafiri mara mbili aliagiza mbunge DK Mary Nagu kuhojiwa na polisi lakini sasa wamemaliza tofauti zao.

Mara ya mwisho ilikuwa wiki iliyopita Msafiri alipoagiza DK Nagu ahojiwe kwa madai ya kuichonganisha serikali na wananchi.

Hata hivyo, Mwisho ni mwa wiki viongozi hao walikutanishwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti baada ya kikao cha kamati ya ushauri kwa ajili ya kumaliza tofauti zao. Msafiri akizungumza juzi akiwa na DK Nagu walipokuwa wakisubiri Mnyeti azungumze na kamati ya siasa ya CCM ya wilaya hiyo alisema hawana tofauti yoyote.

“Mimi na mama yangu DK Nagu hatuna tatizo lolote ndiyo sababu mnatuona hapa tupo pamoja kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Hanang,” alisema Msafiri.

DK Nagu alipongeza kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL) kwa kuandika ipasavyo bila upendeleo kuhusu ttukio hilo.

“Ninyi watu wa Mwananchi mliandika vinzuri juu ya tukio hilo bila ubaguzi au kuongeza chumvi nawapongeza kwa hilo,” alisema.

Mbali na DK Nagu, mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hannang, Mathew Darema pia alihojiwa katika kituo cha polisi Katesh akidaiwa kuchonganisha Serikali na wananchi.

Msafiri alisema aliagiza viongozi hawa wawili wakamatwe na polisi kutokana na kile alichoeleza kuwa waliendelea na mikutano aliyoipiga marufuku.

Julai mwaka jana, dk Nagu ambaye alikuwa waziri katika serikali iliyopita na baadhi ya viongozi wa CCM walipelekwa kuhojiwa polisi baadhi ya kuibuka vurugu kwenye kikao kilichohudhuriwa na Msafiri. Katika tukio hilo, mbunge huyo aliyekuwa katibu wa CCM wilayani humo, Othman Dunga walichukuliwa na polisi wakidaiwa kusababisha vurugu kwenye kikao hicho cha kamati ya siasa ya wilaya hiyo ambako walitoa maelezo na kuachiwa.

Kommentit


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page