PAA LA JIKO LAANGUKIA WANAFUNZI 16 LUSHOTO
- Fahari News
- Mar 12, 2018
- 1 min read

Wanafunzi 16 wa shule ya Sekondari Kihiti iliyopo kata ya Lushoto mkoani Tanga, wamedondokewa na paa la jiko walilokuwa wamejikinga wasinyeshewe mvua.
Kutokana na kuangukiwa na paa hilo, wengi walipatwa na mshtuko mkubwa hali iliyosababisha kulazwa hospitali.
Paa hilo lilidondoka kutokana na kuezuriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali juzi.
Wengi wa wanafunzi hao, walikimbizwa zahanati ya Vuga kwaajili ya kupatiwa matibabu, kisha baadhi yao kuruhusiwa.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe na kusema lilitokea Machi 8, mwaka huu saa 8:45 mchana katika kijiji cha Kihitu wilayani Lushoto.
Alisema tukio hilo liligunduliwa na mwalimu wa shule hiyo, Godfadher Zakayo (32), baada ya kusikia kelele nyingi na kulazimika kuomba msaada kwa majirani.
Alisema baada ya kutokea tukio hilo, wanafunzi hao walifikishwa zahanati ya Vuga kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na baadhi yao kupata mshtuko uliosababishwa na paa.
Alisema kati ya wanafunzi 14 walitibiwa na kuruhusiwa, isipokuwa wawili bado wanaendelea na matibabu, huku mmoja akihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.
Aliwataja aliyehamishwa kuwa ni Halima Karata, wakati mwenzake Sayuni Ukoko ambaye anasoma kidato cha pili amebaki Vuga.
Комментарии