top of page

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAFANIKISHA KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI NA SILAHA.

  • David
  • Mar 5, 2018
  • 2 min read

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga.(Picha David Nyembe wa fahari News Mbeya)

Baadhi ya vifaa ambavyo walikuwa wanavitumia .(Picha David Nyembe wa fahari News Mbeya)

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga akiwaonyesha Vijana ambao walifanya tukio la kupola silaha kwa mlinzi wa kituo cha mafuta cha manyanya na kumkatakata kwa mapanga.(Picha David Nyembe wa fahari News Mbeya)

watuhumiwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamata watuhumiwa mbalimbali wa uhalifu, silaha na vifaa mbalimbali vya kutengenezea silaha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 03.03.2018 majira ya saa 18:30 jioni liliendelea na msako mkali uliofanyika huko maeneo ya Itezi – Uyole, Kata ya Itezi, Tarafa ya Iyunga hapa Jijini Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watu watano [05] wakiwa na Silaha bunduki aina ya Pump Action Shortgun yenye namba 009009906-MP-18EM-M mali ya SUMA JKT ikiwa imefichwa nyumbani kwenye Stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali.

Watuhumiwa waliokamatwa wamefahamika kwa majina ya:-

  1. HAMIS SHABAN [19] Mkazi wa Itezi

  2. IBRAHIM MBILINYI [22] Mkazi wa Itezi

  3. STAN WEMA [21] Mkazi wa Uyole

  4. BAHATI LAULENDI [22] Mkazi wa Iduda

  5. SAMBAA SAMSON [32] Mkazi wa Isyesye

Watuhumiwa baada ya kupekuliwa walikutwa na silaha nyingine ambazo ni:-

  1. Mapanga matatu [03].

  2. Maganda matatu tupu ya risasi

Mnamo majira ya saa 01:30 usiku wa kuamkia tarehe 26.02.2018 huko maeneo ya Kituo cha Mafuta kiitwacho MANYANYA kilichopo Uyole, Kata ya Nsalaga, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, watu wasiofahamika majina walimvamia mlinzi wa SUMA JKT aitwaye CHEWE WILSON [34] Mkazi wa Iduda, Mlinzi wa Suma JKT akiwa lindoni katika Kituo cha mafuta cha MANYANYA kilichopo Uyole na kisha kumjeruhi mlinzi huyo kwa kumkata kwa panga sehemu za kichwani na mguu wa kulia na kisha kumpora silaha bunduki aina ya Shortgun mali ya SUMA JKT na kutoweka nayo.

Na mnamo tarehe 01.03.2018 majira ya saa 06:00 asubuhi CHEWE WILSON [34] alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na majeraha aliyoyapata sehemu ya kichwani na mguu wake wa kulia.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano [05] ambao baada ya kuhojiwa wamekiri kuhusika katika tukio hilo. Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria mara baada ya Upelelezi kukamilika.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page