top of page

JESHI LA POLISI MBEYA LAWATIA NGUVUNI WATENGENEZAJI WA SILAHA KINYUME CHA SHERIA

  • David
  • Mar 5, 2018
  • 2 min read

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga.akiwaonyesha watuhumiwa ambao ndio wataalamu wa kutengeneza silaha za kienyeji(Picha David Nyembe wa fahari News Mbeya)

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga akiangalia moja ya silaha ambayo ni ya kienyeji.

Watuhumiwa ambao ni wataalamu wa kutengeneza bunduki za kienyeji (Picha David Nyembe wa fahari News Mbeya)

Mnamo tarehe 03.03.2018 majira ya saa 12:00 mchana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na misako mikali katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya. Katika msako uliofanyika huko Kitongoji cha Kibaoni, Kijiji na Kata ya Kambikatoto, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watu wawili wakiwa na bunduki aina ya Shortgun iliyotengenezwa kienyeji pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengenezea bunduki.

Watuhumiwa waliokamatwa wamefahamika kwa majina ya:-

  1. FADHILI MAYEGA [60] Mkazi wa Kambikatoto

  2. MASHAKA SAMWEL [38] Mkazi wa Kambikatoto

Aidha baada ya watuhumiwa kupekuliwa walikutwa na bunduki hiyo pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengenezea bunduki aina ya shortgun za kienyeji ambavyo ni:-

  1. Mkono wa kuwekea risasi kwenye bunduki [Cocking Handle]

  2. Unga wa Baruti wenye uzito wa gramu moja.

  3. Mafuta ya kusafishia bunduki

  4. Risasi 25 zilizotengenezwa kienyeji

  5. Tupa 10

  6. Chuma kimoja cha kukatia risasi

  7. Tindo za kukatia mawe

  8. Vipande vya vyuma viwili [02]

  9. Visu vitano [05]

  10. Nyundo kubwa mbili.

  11. Praise moja

  12. Bisibisi moja

  13. Mguu wa Pedal ya Baiskeli

  14. Triger 2

Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria mara tu baada ya upelelezi kukamilika.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha tamaa ya kupata mali kwa njia zisizo halali kwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato.

Aidha Kamanda MPINGA anatoa onyo kali kwa yeyote atakaye jihusisha na uhalifu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lipo imara kuhakikisha usalama wa raia na mali zao na halitasita kumkamata na kumfikisha Mahakamani mtu/watu au kikundi cha watu watakaojihusisha na uhalifu kwa hatua zaidi za kisheria.

Pia Kamanda MPINGA anaendelea kuomba ushirikiano kwa raia wema, viongozi wa mitaa kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page