FURSA MPYA UCHUMI KWA WAKAZI MTWARA
- David
- Mar 5, 2018
- 2 min read

Meli kubwa na za kisasa aina ya Panamax zitaaza kuhudumia katika Bandari ya Mtwara mwakani, mara baada ya kukamilika kwa ujezi wa gati namba mbili hivyo kutoa fursa za kiuchumi kwa wakazi wa mkoa huo wenye uwezo.
Gati hili linalokadiriwa kugharimu sh. Bilioni 137 linajengwa kwa ubia baina yak am mbili za china Railways Major Bridges Engineering Group co.Ltd (CRMBEG) NA China Railways Construction Engineering Group (CRCEG) chini ya usimamizi wa kampuni ya Kijerumani ya INROS LACKNER.
Akiwa mtwara Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, aliagiza kukamilika haraka kwa ujenzi wa mradi huo ili kuwezesha meli kwa ujenzi wa mradi huo ili kuwezehsa meli hizo kutia namga bandalini hapo.
“Mradi una maana kubwa sana kwa upande wa serikali na TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari) kwa ujumla na tunahitaji ukamilike kwa haraka ili kuongeza nafasi ya bandari ya mtwara,” alisema Prof. Mbarawa.
Waziri huyo alisema ujio wa meli hizo katika bandari hiyo ni faraja kubwa kwa wanamtwara kwa kuwa zitachochea kukua kiuchumi kwa mkoa na kuongeza mapato ya serikali.
Katika kuhakikisha mradi wa ujenzi wa gati hiyo unakamilika kwa wakati, Prof. Mbarawa alitaka TPA kusimamia ujenzi wa mradi huo.
Kiongozi huyo wa serikali alisema atarejea tena katika Bandari ya Mtwara kukagua mradi huo ndani ya miezi mitatu kuona maendeleo ya ujenzi na jinsi muda wa kukamilika kwa mradi huo unavyozingatiwa.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Karim Mattaka, alisema ujenzi wa gati namba mbili umefikia asilimia 15.
“Kwa sasa mradi wa ujenzi wa gati namba mbili ya Bandari hii ya Mtwara umefikia asilimia 15 na upo katika hatua ya mwisho mwisho ya usanifu wa gati lenyewe,” alisema Matta.
Kuhusu maagizo ya waziri, Matta alisema TPA imeyapokea kwaajili ya utekelezaji na watamsimamia mshauri na mkandarasi kwa karibu zaidi kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.
Naye Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Nelson Mlali alisema mradi huo ni ukombozi kwa mikoa ya kusini na Tanzania kwa ujumla.
Mlali alisema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uwezo wa bandari ya Mtwara kwa kuwaa kwa sasa imefikia asilimia 93 ya uwezo wake wa kuhudumia shahana.
Alibainisha kuwa katika kipindi cha mienzi minne (Julai 2017-Februari 2018) jumla ya meli 61 zilihudumiwa na bandari hapo. Kati yake, 45 ni za kimataifa na 16 za mwambao.
Bandari ya Mtwara ni kati ya bandari tatu kubwa zilizo katika pwani ya Bahari ya Hindi nchini. Inauwezo wa kuhudumia makasha 200,000 na shehena mchanganyiko tani 400,0000 kwa mwaka. Nyingine ni Dar es salaam na Bandari ya Tanga.
Comments