top of page

MBUNGE  NUSURA AKWAMISHE BAJETI HALMASHAURI MUFINDI

  • Fahari News
  • Feb 28, 2018
  • 1 min read

Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mahamuod Mgimwa, ameshangazwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuendelea kuweka katika bajeti ujenzi wa jingo la zahanati ya Ihalimba badala ya kusema kuwa hicho ni kituo cha afya kama vilivyo malengo yao.

Mgiwa anatoa kauri hiyo wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya halmashauri hiyo juzi ambayo imetengewa sh bilioni 62. Mbunge huyo alitishia kugoma kupitisha bajeti hiyo kutokana na sababu ya kutowekwa wazi wodi itakayojengwa katika kituo cha afya au zahanati.

Alisema katika kikao chao cha ndani cha kamati, walijadiliana kuwa katika zahanati hiyo kuifanya kuwa kituo cha afya

Alisema mtu akipitia bajeti hiyo hata jua kuwa wanalengo la kuwa na kituo cha afya na watashangaza kuona kuwa wanajenga wodi katika zahanati. “Wataalamu mbona mnaenda kinyume cha makubaliano kwasababu tulikubaliana kuwa badala ya kuandika zahanati tutaandika kituo cha afya katika kabrasha lakini nini mmeandika zahanati? Hii haiwezekani , ninaondoa shiringi katika bajeti hii,” alisema Mgimwa.

“Kuna wodi katika zahanati? Mimi nilikuwa naona mkurugenzi aondoe haya maneno na ayarekebishe halafu tuendelee maana akija mtu akasoma hataelewa wodi kwenye zahanati, naomba mrekebishe.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Festo Mgina, alisema watabadilisha lakini katika kabrasha kuandika kituo cha afya wakati ni zahanati pia haitaleta picha nzuri na kusema ushauri ameuchukua na watafanya marekebisho kwa kuwa tayari wamefuatilia kibali cha kuibadilisha kuwa kituo cha afya.

Baada ya mvutano wa muda kidogo, mbunge alikubaliana na kuapisha bajeti hiyo baada ya kukabiliana na kile alichokuwa akiona kimekwenda tofauti katika kabrasha la bajeti.

Comentários


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page