top of page

MASWALI 3 YALIYOMTUPA JELA SUGU

  • Fahari News
  • Feb 28, 2018
  • 2 min read

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite, alitaja maswali matatu yaliyomfanya afikie uamuzi wa kuwatia hatiani Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mwenzake.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, walihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Hakimu Mteite alisema kabla ya kufikia uamuzi wake, hata hivyo, Mahakama imeona viini vitatu ambavyo vilitengeneza maswali katika kesi hiyo.

Aliyataja maswali hayo kuwa ni je, maneno yaliyotolewa na washtakiwa kweli yalikuwa ni ya fedheha dhidi ya Rais? Mlengwa katika shauri hilo ni Rais John Magufuli kweli? Na je, washtakiwa walitoa maneno hayo?

Katika dhana hiyo, Hakimu Mateile alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri ni kweli washtakiwa walitoa maneno hayo, na kwamba waliyekuwa wanamsema ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Haya maneno ya washtakiwa kuwa huwezi kupendwa kwa ‘kumshuti’ Lissu, kumteka Ben Saanane, watu kuuawa mchana kweupe na kufungwa kwenye viroba, Rais anatubadilishia aina ya kututawala …. Ni ya kitaifa na yanamuhusu Rais Magufuli ambaye ndiye mtawala,” alisema Hakimu Mteite.

Sababu polisi

Hakimu huyo alisema ushahidi wa upande wa Jamuhuri ambao ulitolewa na willium Nyakomago na Joram Magova ulikuwa na uzito kwa sababu ni polisi ambao walikuwepo eneo la tukio na sauti iliyotolewa mahakamani kama kielelezo ilikuwa ni ya washtakiwa.

Aidha, Hakimu Mteite aliiambia mahakama ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi ulikuwa hauna nguvu.

Alisema mshtakiwa namba mbili, Masonga alikana mbele ya Mahakama na kuwepo kwenye kutano

Siku hiyo hakuna kielelezo alichotoa mahakamani hapo kuthibitisha hivyo mahaka haikutambua utetezi huo.

Kabla ya Hakimu Mteite kutoa hukumu hiyo. Wakili wa serikali Joseph Pande aliiomba mahakama kuwapa adhabu kali washtakiwa ili iwe funzo kwa wengine.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala aliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu washtakiwa kutokana na majukumu ya kibunge na kifamilia walionayo.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page