LUKUVI ATAHADHARISHA VISHOKA BOMBA LA MAFUTA LA UGANDA
- David
- Feb 28, 2018
- 1 min read

Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaonya wakazi wa wilaya ya kahama kuwa makini na vishoka.
Alisema vishoka hao wanaweza kujitokeza kuwarubuni kuza ardhi yao kwa bei ya chini na wao kufidia kwa bei kubwa wakati wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga nchini.
Pia amewaonya watakaofanya udanganyifu wa kupanda mimea kwenye maeneo yanayotarajia kupita bomba la mafuta.
Alisema tayari eneo hilo lilishapigwa picha ya angani ambayo imebainisha mimea yote iliyokuwapo na inayostahili kulipwa fidia hivyo watakaongeza watapoteza muda wao.
Aliyasema hayo juzi katika mkutano wa pili wa wadau wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Haima, , Uganda hadi Tanga waliopo wilayani Kahama.
Lukuvi alisema mwenye mamlaka ya ardhi katika nchi hii ni Rais ambaye ndiye mwenye uwezo wa kufuta mmiliki yoyote itakayopita bomba hilo la mafuta.
Alisema watakaofutiwa watalipa fidia kulingana na sheria za mamlaka ya vijiji, mijini na majiji hivyo hakuna atakayepoteza mali yake katika mradi huo.
Naye waziri wa Nishati DK. Medard Kalemani alisema mradi huo wa bomba la mafuta unatarajia kutoa ajira 10,000 za muda na 1,000 za kudumu utaanza utekelezaji wake wa ujenzi mnamo Mei mwaka huu.
Alisema baada ya kukamilika utarajia kusafirisha mapipa ya mafuta ghafi bilioni 1.7.
DK. Kalemani alisema nchini bomba hilo litapita katika mikoa minane ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga yenyewe. Waziri Kalemani aliwataka wananchi wa Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla kuupokea mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack alisema wananchi wa mkoa huo watatoa ushirikiano wa kutosha kwa wafanyakazi na wahusika wa mradi huo.
Комментарии