top of page

KOMBE LA DUNIA KUTEMBELEA NCHI HIZI

  • David
  • Feb 28, 2018
  • 2 min read

Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili. Kombe hilo ambalo liliwasili nchini Kenya na kupokelewa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta lilipata watazamaji wengi ambao walifika kujionea na kupiga picha pamoja na kombe hilo. Raia wa kawaida hawakuruhusiwa kuligusa kombe hilo, na badala yake walilitazama likiwa katika sanduku la Kioo. Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa kombehilo nchini Kenya. Kando na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao huruhusiwa kuligusa. Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni, nchini Urusi. Na ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa nchini Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil. Kabla ya kutua Kenya, kombe hilo lilikuwa nchini Sudan kisha Ethiopia. Hata hivyo ziara ya kombe hilo bado inaendelea ambapo limeondoka nchi Kenya na kuelekea Maputo, Msumbiji. Nchi nyingine za Afrika zinazotarajia kufikiwa na ziara hiyo ya Kombe la Dunia ni Afrika Kusini, Uganda, Nigeria, Senegal, Cote D’Ivoire (Ivory Coast) kisha Misri. Baada ya ziara ya kombe hilo barani Afrika kukamilika, litaelekea barani Ulaya kuendelea na ziara yake kabla ya kuanza mchuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Urusi, Juni 14, mwaka huu. Hapa chini ni ratiba nzima ya ziara ya Kombe la Dunia katika nchi mbalimbali duniani. Zipo nchi ambazo tayari zimeshatembelewa na nyingine zinaendelea kutembelewa. Kituo Tarehe Colombo, Sri Lanka 23-24 January Male, Maldives 24-25 January Phuket, Thailand 26-27 January Vientiane, Laos 28 January Macau, China P.R 29 January Nukualofa, Tonga 31 January Honiara, Solomon Islands 1 February Port Moresby, Papua New Guinea 1 February Lahore, Pakistan 3 February Almaty, Kazakhstan 4 February Bishkek, Kyrgyz Republic 5 February Dushanbe, Tajikistan 5 February Tashkent, Uzbekistan 6 February Ashgabat, Turkmenistan 7 February Yerevan, Armenia 7 February Tblisi, Georgia 8 February Baku, Azerbaijan 9 February Valetta, Malta 10 February Vienna, Austria 11 February Minsk, Belarus 13 February Sofia, Bulgaria 14 February Tel Aviv, Israel 15 February Larnaca, Cyprus 16 February Ramallah, Palestine 17-19 February Amman, Jordan 20 February Dubai, United Arab Emirates 21 February Khartoum, Sudan 22-23 February Addis Ababa, Ethiopia 24-25 February Nairobi, Kenya 26-27 February Maputo, Msumbiji 28 February Johannesburg, Afrika Kusini 1-2 March Cape Town, Afrika Kusini 3 March Kampala, Uganda 5-6 March Abuja, Nigeria 7-8 March Lagos, Nigeria 9-10 March Dakar, Senegal 11-12 March Abidjan, Cote d’Ivoire 13-14 March Cairo, Misri 15-16 March Naples, Italy 17-19 March Paris, France 20-21 March Cologne, Germany 22-23 March Oslo, Norway 24 March Torshavn, Faroe Islands 24-25 March Reykjavik, Iceland 25 March Tucuman, Argentina 27-28 March Berazategui, Argentina 29 March Buenos Aires, Argentina 30-31 March Rosario, Argentina 1-2 April Bogota, Colombia 3-5 April Panama City, Panama 6 April San Jose, Costa Rica 7-8 April Guadalajara, Mexico 9-10 April Monterrey, Mexico 11-12 April Mexico City, Mexico 13-15 April New York, USA 16 April Miami, USA 17 April Los Angeles, USA 18-20 April Frankfurt, Germany 22 April Ulaanbaatar, Mongolia 23 April Beijing, China P.R 25 April Shanghai, China P.R 26 April Tokyo, Japan 27-28 April Osaka, Japan 29-30 April Vladivostok, Russia 1 May

Коментари


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page