SUGU AHUKUMIWA KIFUNGO JELA
- David
- Feb 26, 2018
- 1 min read

Mbunge wa Mbeya mujini Joseph Mbilinyi "SUGU' akiwa na Mke wake mtalajiwa wakiwasili katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwaajili ya kusikiliza hukumu yake dhidi ya uchochezi.Picha na David nyembe wa Fahari News)

Wakili Peter Safari kulia wakijadili jambo na Mwanasheria wa chama hicho, Peter Kibatara mara baada ya kuwasili mahakamani hapo leo.

Mbunge wa iringa mjini Chadema Mchungaji Peter Msigwa akiongea akiangalia moja ya kitabu ambacho akionyeshwa na Wakili Peter Safari leo mapema asubuhi .Picha na David nyembe wa Fahari News)

Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu'amehukumiwa kwenda jela kifungo cha miezi mitano baada ya kupatikana na hatia ya kutoa lugha ya fedheha kwa rais Dr.John Magufuli. Hukumu hiyo imetolewa Leo na hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya Maiko Mteite baada ya kuridhika ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka. Pia mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miezi sita katibu wa chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga kwa kosa hilo. Washtakia hao wanatajwa kutenda kosa la kutoa maneno ya kumfedhehesha raisi Disemba 31 katika viwanja wa Luanda nzovwe wakati wakizungumza na wananchi.
Comments