top of page

VIASHIRIA VYA NGONO VYATAJWA

  • Fahari News
  • Feb 23, 2018
  • 1 min read

Ukatili wa kingono kwa mabinti unaongezeka kwa kasi katika kata ya Arusha Chini na Mabogini, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, huku sinema zinazoonyeswa usiku na wanafunzi kuzurula mitaani muda wa masomo, vikitajwa kuchochea.

Hali hiyo imefichuliwa na Ofisa mradi wa majaribio wa kutokomeza ukatili wa kingono kwa mabinti na ukeketeji kupitia sanaa. Immaculate Mworia, wakati wa kikao cha kushirikisha wadau katika matokeo ya mradi huo.

Mworia alikuwa akizungumza juzi na viongozi wa dini, viongozi wa jadi, wasaidizi wa kisheria, maofisa maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii.

“Tatizo ni kubwa na wasaidizi wa kisheria wameeleza wazi kwamba kata ya Mabogini kesi 12 visababishi ni sinema zinazoonyeshwa usiku pamoja na wanafunzi kuzurura mitaani muda wa masomo,” alisema.

Mradi huu wa mwaka mmoja unatekelezwa na shirika la wanawake la ubadilishanaji wa Habari na Msaada wa kisheria mkoani Kilimanjaro (Kwieco), unaofadhiliwa na Shirika la Physician For Social responsibility (PSR) la Finland.

Kwa mujibu wa Immaculate, baadhi ya wazazi wanatajwa kuwa chanzo kwa sababu huwapaa watoto wao fedha wa ajili ya kuangalia sinema hizo usiki, zinazoonyesha uhusiano wa jinsia yasiyo na maadili. Matokeo ya mradi huo yamebaini kuwa katika Kijiji cha Kirungu huko Arusha chini,wananchi wanakwenda kuangalia sinema usiku kwa sh 200, huku baadhi ya wanafunzi wakidaiwa kwenda kutizama picha ambazo hazina maudhui manzuri.

Katika eneo la Mabogini, Chimbuki la ukatili huo wa kingono limetajwa ni ulevi wa kupindukia, wanafunzi kuzurura muda wa masomo na familia nyingine kupuuza imani ya dini.

Mpaka sasa tathimini ya kupinga ukatili wa Kingono, ukeketaji, ndoa za utotoni na ubakaji inaonyesha mikoa ya kanda ya kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara imechukua nafasi ya pili kitaifa ikiwa ni asilimia 37.8.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page