AFARIKI DUNIA AKIENDA KWENYE MSIBA WA MKEWE
- Fahari News
- Feb 23, 2018
- 1 min read



Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda msibani, kuacha njia na kupinduka katika eneo la kifaru , Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Isah, alithibitisha kutokea ajali hiyo, katika barabara kuu ya Mwanga-Moshi.
Akielezea mazingira ya tukio hilo, Kamanda Issah alisema gari hilo lenye namba za usajili T 329 BZI, aina ya Toyota Noah lilikuwa likiendeshwa na dereva Clemens Kweka (48) likitokea Dar es salaam kwenda Moshi kwenye msiba.
Alisema kuwa liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha mume wa marehemu, kaka wa marehemu na majeruhi watatu.
“Gari hili lilikuwa likitokea Dar es salaam kuja kwenye mazishi huku Moshi, lakini lilipofika maeneo ya Kifaru, Wilaya ya Mwanga liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo wa familia moja.,” alisema.
Kamanda Issah aliwataja waliofariki dunia kuwa ni mume wa marehemu aliyetambulika kwa jina la Semui Kweka (88) na kaka wa marehemu, Dausen Kwayu(70).
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni aliyekuwa dereva wa gari hilo, Clemens Kweka (48), urasa Elipokea (70) na Beti Kweka (43) wote wakiwa ni ndugu wa familia moja na wakazi wa Dar es salaam.
Комментарии