TRA YAINGIA MATATANI KWA TAARIFA YA KANISA LA ASKOFU KAKOBE, YATOA UFAFANUZI
- David
- Feb 22, 2018
- 1 min read

Dar es salaam, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejikuta matatani baada ya wadau, maofisa wa benki na viongozi wa dini kuhoji uhalali wa mamlaka hiyo kuweka hadharani taarifa za fedha za kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF). Juzi, TRA ilitoa taarifa ya uchunguzi uliofanyika kuhusu kauli ya kiongozi wa kanisa hilo Askofu Zachary Kakobe aliyoitoa wakati wa ibada ya mkesha wa Krismasi mwishoni mwa mwaka jana kuwa ana fedha nyingi kuliko serikali.
Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere alisema wangefanya uchunguzi kuhusu kauli hiyo, lakini taarifa aliyotoa juzi ilionyesha kuwa Askofu Kakobe hana akaunti katika benki yoyote nchini bali ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti ya kanisa analoliongoza. Kichere alisema akaunti za kanisa hilo zipo katika benki ya NBC zikiwa ni zaidi y ash 8 bilioni na zinatokana na fedha za sadaka, zaka na changio zinazotolewa na waumini. Kichere alipotafutwa jana kuhusu hatua ya kutangaza taarifa za kifedha za kanisa hilo alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari inaeleweka na inajieleza hivyo hawezi kutoa maoni zaidi.
“Wakati nataka kufanya uchunguzi nilieleza wazi nia yangu, hata baada ya kumaliza uchunguzi niliona ni busala kusema yaliyobainishwa katika uchunguzi, sitaki ‘ku-comment’ (Kutoa maoni) zaidi, mjadala wa masuala ya Kakobe ulishafungwa,”
amesema Kichere. Akizungumzia taarifa ya TRA , ofisa mwandamizi wa benki moja nchini ambaye hakutaka utambulisho wake uwekwe hadharani alisema kitendo cha mamlaka hiyo kutoa taarifa za fedha kwa umma ni uvunjifu wa sheria. Alisema kwa mujibu wa sheria taarifa za kibenki zinapokuwa zinahitajika na vyombo au mamlaka za serikali zinaweza zikatolewa mahakamani, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa au polisi lakini si kwa umma.
Comments