AJALI YA BAJAJI YAUA MTU MMOJA MBEYA.
- David
- Feb 21, 2018
- 1 min read

wananchi wakiangalia Bajaji iliyogongwa jana usiku maeneo ya Soweto.Picha David Nyembe wa Fahari News



Gari aina ya Pajero iliyogonga Bajaji na kusababisha kifo cha Mtu Mmoja Picha David Nyembe wa Fahari News

Polisi Usalama Barabarani wakibeba mwili kupakia kwenye gari mara baada ya ajali kutokea Picha David Nyembe wa Fahari News

Mtu Mmoja Amefariki Na Wengine Wawili Kujeruhiwa Katika Ajali Iliyohusisha Bajaji Yenye Namba Za Usajili MC604 AGD Iliyogongwa Na Gari Aina Ya Pajero Yenye Namba Za Usajili T575 CQV Katika Eneo La Mama John Mjini Mbeya Hapo Majira Ya Usiku.
Mashuhuda Wa Ajali Hiyo Wesema Chanzo Cha Ajali Hiyo Ni Dereva Wa Gari Aina Ya Pajero Kupiliza Akiwa Barabara Kuu Licha Ya Kuona Dereva Wa Bajaji Akionesha Ishara Ya Kuingia Barabara Kuu,Ambapo Aliigonga Bajaji Hiyo Na Kusababisha Kifo Pamoja Na Majeruhi Wawili.
Kwa Upande Wao Madereva Wa Bajaji,Wamesema Tangu Kutolewa Kwa Agizo La Kusitisha Babaji Barabara Kuu,Imekuwa Kawaida Kwa Madereva Wa Magari Madereva Wa Magari Makubwa Kudharau Bajaji Zikiwa Barabarani Kwa Kuona Hazina Haki Na Hivyo Kuendelea Kusababisha Ajali Ambazo Zinaweza Kuepukika.
Hata Hivyo Wamelitupia Lawama Jeshi La Polisi Kitengo Cha Usalama Barabarani Kwa Kutofuatilia Taarifa Za Madereva Babaji Kugongwa Mara Kwa Mara na kupoteza maisha ya watu Lakini Wahusika Hawachuliwi Hatua Zozote.
Comments