MATUTA YAMKERA NAIBU WAZIRI UJENZI
- Fahari News
- Feb 19, 2018
- 1 min read

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchunguzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amekerwa na wingi wa matuta katika barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga.
Nditiye alionyesha kukerwa na matuta hayo jana, baada ya kuwasili na kupokea taarifa ya Mkoa wa Rukwa ambapo yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua shughuli za maendeleo.
Alisema kuweka matuta mengi kunachangia kuharibu miundombinu ya barabara pamoja na magari hasa pale yanapopunguza mwendo ili kupita, hivyo kutodumu muda mrefu.
Naibu waziri huyo alisema atawasilisha suala hilo kwa waziri wa ujenzi ili waone namna ya kutatua changamoto hiyo kwa kuwa inalalamikiwa na wamiliki wa vyombo vya usafiri, madereva na wananchi kwa madai kuwa matuta yanawafanya safari kuchukua muda mrefu. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga,
DK. Halfan Haule aliwahi kunukuliwa akitaka kuondolewa kwa matuta hayo, ambapo alidai kwamba wamekuwa wakitumia muda wa saa tano hadi saba kutoka Sumbawanga hadi Tunduma umbali wa kilomita 220.
Alisema wingi wa matuta hauna manufaa kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa kuwa ni sawa na ilivyokuwa siku za nyuma wakati ikiwa ni barabara ya vumbi. Barabara hiyo inakadiliwa kuwa na matuta zaidi ya 1000 na yamekuwa yakilalamikiwa na watumiaji wengi
Comentários