WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MWENYEKITI WA CWT SINGIDA
- Khalidi
- Feb 11, 2018
- 1 min read
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Akiwa hospitalini hapo Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Mwenyekiti huyo na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo wakihudumiwa vizuri.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa alipomtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es salaam. kulia kwa Waziri Mkuu ni Daktari Bingwa wa Moyo Dr Sulender Kuboja.
Pia Waziri Mkuu amewajulia hali mabinti pacha walioungana Consolata na Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwakatika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba Serikali inadhamira ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku
Kwa upande wake, Mwalimu Jumbe alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali. Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa taasisi ya JKCI kwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.
Kwa upande wao Maria na Consolata walishukuru kwa msaada wa huduma za matibabu wanazozipata na kwa sasa wanaendelea vizuri. Pia walimshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kuwajulia hali na kumtakia kheri katika shughuli zake

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewajulia hali mabinti pacha walioungana Consolata Mwakikuti na Maria Mwakikuti ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).Jijini Dar es salaam.
Comentarios