WENYE KUIDAI SERIKALI WAHAKIKISHIWA MALIPO
- Fahari News
- Feb 8, 2018
- 1 min read

Serikali imesema wafanyakazi wa serikali na wazabuni wanaoidai watapewa stahiki zao karibuni kwani ipo katika hatua za mwisho za uhakiki wa madeni hayo.
Fedha hizo sh.bilioni 200 zilizoahidiwa na Rais Magufuli Januari 3, mwaka huu, alipokutana na Gavana wa Benki Kuu (BoT). florens Luoga, Ikulu jijini Dar es salaam.
Msemaji Mkuu wa serikali, Hassan Abbas aliyasema hayo jana wakati akitoa taarifa ya kula mwenzi ya serikalimbele ya waandishi wa habari. “Tayari fedha zimekabidhiwa Wazara ya Fedha na Mipango, lakini kwa taratibu za serikali lazima uhakika ufanyike, kwa sasa uko kwenye hatua za mwisho na zitaaza kulipwa wakati wowote,” alisema.
Alisema fedha hizo zitalipa watumishi wenye madai ya likizo, safari na mengineyo ambayo yamehakikiwa na pia wazabuni wanaodai serikali kama ambavyo Rais alisema.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, angeweza kutoa mapema fedha hizo lakini aliona kuna umuhimu wa kuhakiki madeni husika.
“Nina uhakika zitawasaidia wananchi ambao walikuwa waaminifu, waliokuwa wadhabuni, zitahakikisha wenye madeni ya ukweli na sio uongo kupata fedha za kuwasaidia kufanya biashara,” alisema Rais Magufuli siku hiyo.
Aidha alimwingiza Gavana kushirikiana na wizara ya Fedha na Mipango ili wanaodaiwa serikali wenye madeni ya ndani na sio ya nje na kwamba ni njia kw kuwa ni njia ya kukuza uchumi kwa kuwa bilionea 200 zitasambaa kwa wananchi.
Comments