MKUU WA KKT AWATAKA WASHARIKA MTWARA KUWA WATULIVU
- Fahari News
- Feb 6, 2018
- 1 min read

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKT), Askofu Fredrick Shooamewataka washarika wa Kanisa Kuu Mtwara kuwa na subira wakati akijiandaa kwenda kuzungumza nao. DK. Shoo, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaziskazini alisema jana kuwa amepanga kwenda kuwaona kama walivyoomba, lakini akawataka wadumishe upenda na kumtumikia Mungu kama Wakristo wamoja.
Alisema hayo alipozungumza ikiwa ni siku moja baada ya Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, DK Lucas Mbedule kuwaomba msamaha washarika wa kanisa hilo la Mtwara.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakimpangia Askofu huyo kwa takribani miaka miwili lakini juzi DK Mbedule aliwaangukia na kuwaomba msamaha wote aliowakosea ili wasiliumize kanisa. “Nimewakosea mengi siwezi kuhesabu kabisa. Mimi ni mwenye dhambi kabisa kabisa sistahili kabisa. Naomba mnisamehe tusilitese kanisa
“Nimewakosea mengi siwezi kuhesabu kabisa. Mimi ni mwenye dhambi kabisa kabisa. Naomba mnisamehe tusilitese kanisa. Kama kunajambo njoo tuzungumze,” alisema DK Mbedule.
Akiwa katika ibada juzi, askofu huyo alisema watakapoweka vinzuri utaratibu, DK Shoo atakwenda kuwasalimia na kuzungumza nao kwa kuwa mazungumzo yanaruhusiwa ila yasiharibu utaratibu.
Kabla ya kutoa kauli hiyo, msaidizi wa Askofu, Mchungaji Yeriko Ngwema alimuita mmoja wa waumini, Steven Macha ambaye alimtaka askofu kuitisha majadiliano ili kumaliza mgogoro huo.
Commenti