top of page

KAGERA SUGAR HALI SI SHWARI

  • Fahari News
  • Feb 1, 2018
  • 1 min read

Wakati taarifa za kunyapia zikisema kuwa baadhi ya wachezaji wa Kagera Sugar akiwamo nahodha George Kavila na kipa Juma Kaseja hawaivi chungu kimoja na timu hiyo iliamua kukaushia mazoezi ya jana Jumatano na kukaa kikao kizito.

Kagera Sugar inamwenendo mbovu katika Ligi Kuu Bara kwa kupata matokeo mabaya na ilitolewa kwenye michuano ya Kombe la FA hivyo jana Jumatano waliamua kuacha kufanya mazoezi na kufanya kikao kizito kilichochukua masaa mawili kuanzia saa 2 asubuhi.

Wachezaji wote walifahamu kwamba wanakwenda uwanjani kwaajili ya mazoezi ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC itakayochezwa CCM Kirumba, lakini hali ilikuwa tofauti walipofika uwanjani kwani waliishia kufanya kikao tu.

Chanzo chetu kinasema kikao hicho kilichukua muda mrefu ili kupata suluhisho la matokeo mabaya wanayopata ambapo amedaiwa kukabiliana kwa pamoja kujituma na upambana katika mechi zijazo ili kujinusulu kwenye hatari ya kushuka daraja. Hivyo hadi muda unafika ambao ni wa kumaliza mazoezi walijikuta ndio wanamaliza kikao chao hicho.

Kagera Sugar ambayo ipo chini ya kocha Mecky Mexime inatarajiwa kuondoka Bukoba leo Alhamisi asubuhi kuelekea Mwanza ikiwa imekusanya pointi 13 katika mechi zake 15 za raundi ya kwanza na kushika nafasi ya 13 katika msimamo.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page