Kijiji chavamiwa na kundi kubwa la Fis
- Khalidi
- Jan 31, 2018
- 1 min read

Wananchi wa Kata ya Inyeze wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekuwa wakiishi kwa hofu kutoka na kuwepo uvamivi wa kundi kubwa la fisi katika maeneo ya kijiji chao
Hali hiyo imewafanya wananchi hao kuishi kwa mashaka huku hofu kubwa ikiwatanda juu ya watoto wao kwani fisi hao wamekuwa wakiingia kijijini hapo majira ya usiku na mchana
Wananchi wa kijiji hicho wamepaza sauti zao kwa diwani wa kata hiyo Lucas Makulumo kutoka na hali hiyo hatairshi kwa maisha yao Diwani wa kata hiyo amefikisha malalalmiko hayo kwenye baraza la madiwani na kuitaka halmashauri kupitia kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abel Shija, aeleze halmashauri ina mpango gani juu ya wanyama hao waliovamia kata yake na kuhatarisha maisha ya wananchi wake. Aidha diwani huyo alilieleza baraza hilo kuwa matukio ya wanyama hao kuvamia maeneo ya kata yake yamekuwa ya kawaida, hali inayowatia hofu wananchi wake, wakiwamo watoto wanakwenda shule.
Mwenyekiti Shija alimuagiza mkurugenzi kuhakikisha anawatumia wataalamu wa maliasili na wanyamapori kuhakikisha wanyama hao kuondolewa na kuhakikisha hawaleti madhara kwa wananchi.
Comments