top of page

MGOGORO KUMFIKIA MAGUFULI

  • Fahari News
  • Jan 25, 2018
  • 2 min read

\

Mgogoro wa mpaka kati ya kijiji cha Lekrumuni wilayani siha na mbuga ya wanyama ya ‘End C’ utapelekwa kwa Rais John Magufuli kwa utatuzi, katibu wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Humprey Polepole aliahidi juzi.

Mbuga hiyo yenye ukubwa wa hekali zaidi ya 3,500 za Malisho ya wanyama, inamilikiwa na kampuni ya Rachi za Taifa (NARCO).

Polepole alijitwika mgogoro huo na kudai suala hilo ni kama limwkwishapatiwa ufumbuzi wa kudumu, akiwa eneo la Ndinyika wilaya ya Siha, wakati akimnadi mgombea Ubunge wa CCM DK. Godwin Mollel.

“Mkitupatia huyu kijana (DK. Mollel) awe Mbunge wa Siha, mgogoro huu ni kama umekwisha,” alisema polepole. “Nimelibeba jambo hili na ninakwenda kuzungumza na Mheshimiwa Rais (Magufuli) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.”

“Litakwisha kabisa muda mfupi ujao, hilo naahdi kabisa.”kabla ya polepole kukubali kushughulikia mgogoro huo, DK. Mollel alimweleza katibu huyo wafugaji wa jamii ya Kimasai waliopo katika ukanda huo wa mbuga ya End C wanaomba serikali igawe ardhi hiyo na kutenga eneo la ranchi ya malisho ya mifugo, ili kumaliza mgogoro kati yao na wamiliki wake.

Polepole alisema kutokuwapo kwa mahusiano mazuri baina ya wawakilishi wa wananchi kutoka vyama vya upizani na watendaji wa serikali kuesababisha kero za wananchi kushindwa kutatuliwa kwa wakati.

Mollel anagombea tena kiti hicho baada ya kujiudhulu Ubunge wake Desemba 14, mwaka jana na kujiunga na CCM, baada ya kuchaguliwa mwaka 2015 kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo .

Anachuana vikali na mgombea wa Chadema, Elvis Mosi na Tumsifuel Mwanri wa Chama cha wananchi (CUF).

Polepole alimwahidi DK. Mollen kwamba kwa sasa kero za wafugaji wa jamii ya kimasai kutoka maeneo ya ufugaji wa jamii ya kimasai kukosa maeneo ya ufugaji zitatatuliwa kwa sababuamejiunga na chama kilichounda serikali.

コメント


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page