top of page

DC AINGIA MATATANI KWA KUPIGA KAMPENI

  • Khalidi
  • Jan 23, 2018
  • 1 min read

itendo cha Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu kupanda jukwaani kumnadi mgombea wa CCM katika Jimbo la Siha, Dk Godwin Mollel kimechafua hali ya hewa baada ya kupingwa na vyama vya siasa huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikisema hakufanya jambo sahihi. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima ameliambia Mwananchi jana kuwa ili Buswelu aweze kuchukuliwa hatua, wenye jukumu la kumshtaki ni vyama vinavyopinga jambo alilolifanya. Alisema vyama hivyo vinatakiwa kumshtaki katika kamati ya maadili inayoundwa na wajumbe wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi katika jimbo husika na kwamba jambo hilo linapaswa kufanyika ndani ya saa 72, tangu apande jukwaani. Wakati DC huyo akiibua kizazaa hicho, CCM imeendelea kumnadi Dk Mollel huku katika Jimbo la Kinondoni, wagombea ubunge wa CCM, Chadema na Sau wakiwekewa pingamizi. Uchaguzi wa Siha na Kinondoni utafanyika Februari 17 na unavishirikisha vyama 12, huku ukitajwa kuwa ni mpambano mkali baina ya CCM na Chadema inayoungwa mkono na vyama vitano vya Ukawa ambavyo ni NLD, NCCR-Mageuzi, CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad na Chaumma iliyojiunga hivi karibuni. Uchaguzi huo unafanyika baada ya waliokuwa wabunge; Mollel (Siha- Chadema) na Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF) kujivua uanachama wa vyama hivyo kwa maelezo kuwa wanamuunga mkono Rais John Magufuli na baadaye kujiunga CCM. Chama hicho tawala kimewapitisha wawili hao kutetea majimbo hayo, huku Chadema ikimsimamisha naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu (Kinondoni) na Elvis Mosi (Siha).

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page