MABASI 400 YAFUNGWA ‘VING’AMUZI’ MWENDO
- Fahari News
- Jan 18, 2018
- 1 min read

Mamlaka ya usafiri wanchi kavu na Majini (Sumatra), imefunga Ving’amuzi kwenye mabasi 409 ya mikoani na nje ya nchi, ili kuthibiti mwendokasi na kupunguza askari wanaosimama barabarani kuyafuatilia.
Aliyebainisha maendeleo ya hatua hiyo ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Sumatra, Johansen Kahatano, ambaye alisema tangu mwaka 2016 magari 409 yamefungwa kifaa ambacho kinaonekana makao makuu ya jeshi la polisi na Sumatra ili kufuatilia mwendo wa magari.
Alisema ufungaji wa vifaa hivyo ni kwa mujubu wa sheria na umekamilika kwa magari yaendayo kanda ya ziwa, na kutoka kanda hiyo kwenda Kaskazini na sasa wanashughulikia ufungaji kwa magari ya kwenda kanda ya kati ya mikoa ya Dodoma na Singida.
Alisema ameamua kutumia na mfumo huo baada ya vithibiti mwendo kushindwa kufanya vinzuri kwani madereza walivichezea kwa kuwa vilitegemea umeme wa gari ba kuungwa kwenye gia ‘box’ hivyo kutoa nafasi ya kuvichezea ili visisome mwendo.
“Wakati wa vithibiti mwendo ilikuwa dereva akizidisha mwendo gari inakata mafuta na haiwezi kuendelea na safari, pia alitumia mfumo wa umeme wa gari, hivyo wengi wa madereva wakiwemo ‘switch’ nyingine wanakimbia wakikutana na polisi ndiyo wanarejesha,” alisema katika mahojiano na Redio One jana.
“Ilikuwa ni kazi ngumu kwa Jeshi la polisi kwa kuwa ili kuwabaini ni hadi waendeshe gari husika au kufuatilia mfumo wa nyaya za umeme ili kujua kama ziko sawa au la, ugumu huo ulisababisha wachezee mfumo huo kwa kiasi kikubwa sana.”
Comments