top of page

HATIMA YA MALIPO VYETI FEKI YAIVA

  • Khalidi
  • Jan 18, 2018
  • 1 min read

Hatima ya mafao ya wafanyakazi wa serika walioondolea kwenye ajira kutokana na kubainika kuwa ana vyeti feki itajulikana kabla ya Bunge la Bajeti imefahamika.

Hatua hiyo inatokana na serikali kujibu hoja nane za shirikisho la vyama vya wafanyakazi tanzania (Tucta) na kwamba suala la kulipwa au kutolipwa haki zao litafahamika Machi au Aprili, mwaka huu.

Hoja nyingine ni ajira kwa waliomaliza darasa la saba, kupandishwa madaraja, madeni ya wafanyakazi, nyongeza za mishahara, kutofanyika vikao vya bodi, kujua idadi ya taasisi zilizoundwa na kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Katibu Mkuu wa Tucta. DK. Yahya Msigwa, alisema jana jijini Dar es salaam kuwa mamlaka mbalimbali zinamalizia kulifanyia kazi suala la vyeti feki na kwamba kabla ya mei Mosi, mwaka huu, hatima yao itakuwa imepatikana.

“Unajua kilichofanyika ni kosa la jinai na la kinidhamu, hivyo sisi Tucta tunaendelea kuiomba serikali angalau wapatiwe kifuta machozi,”alisema.

Alisema ajira kwa waliomaliza darasa la saba serikali ilitoa waraka unaosema watumishi wa umma wanapaswa kumaliza elimu ya kidato cha nne kuazia Mei 20,2004.

Pia alisema baada ya hapo, walitakiwa kujiendeleza ili kuwa na vigezo vya kuendelea kuwa watumishi wa umma iwapo zipo baadhi ya idara zinawahitaji kujenga hoja.

Alisema malipo yataaza tangu siku ya kupata barua ili ili kupunguza madeni ambayo inadaiwa na kwamba kimsingi katika hilo, yako madeni ya mishahara na isiyo ya mishahara.

Kuhusu madeni kwa mujibu wa DK. Msigwa, serikali imesema imemaliza uhakiki na imeanza kulipa lakini itakuwa vigumu kulipa watu wote kwa mkupuo bali watazingatia uhakiki wa madeni yenyewe.

Comments


Top Stories

Join our mailing list

Never miss an update

© 2017 Fahari News 

bottom of page