WALIOTOKA KWA MSAMAHA WA RAIS WAPEWA ONYO KALI NA POLISI.
- Khalidi
- Jan 17, 2018
- 2 min read

Jeshi la polisi limetoa onyo kwa wahalifu waliopata masamaha wa Rais kuwa iwapo watarudia kufanya vitendo vya uhalifu, watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa alisema taarifa za kiintelejensia zinaonyesha kuwa baadhi ya waliotoka gerezani kwa msamaha wa Rais wanatumiwa na wenzao ambao wapo gerezani na kuwaelekeza waende sehemu Fulani kuchukua silaha na watakapozifanyia kazi wawapelekee posho
Alisema askari waliweka mtego na kufika eneo la nyumba kwa mzee Saidi Omary (62) kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na silaha aina ya AK 47 yenye namba UC 49331998 ambayo haikuwa na magazine yake
Mambo sasa aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Ally Makwaya (40) na Fedrick Odhiambo (50) wote wakaziwa Tandale kwa Tumbo
Walipohojiwa kuhusu wapi walipata silaha hiyo walisema shughuli zao kubwa ni kuokota makopo na Vyuma chakavu na kuwa hata silaha hiyo waliokota kwenye karakana ya magari (Gereji) Kinondoni Mwinyijuma
Aidha alisema watuhumiwa hao walieleza kuwa baaada ya kuokota silaha hiyo hawakutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi, hivyo waliamua kutafuta mteja wamuuzie ili wapate hela za kujikimu
Alisema silaha waliookota ni silaha kubwa na ni toleo la mwanzo , na wahusika wakati wanajitetea walisema wameitoa kwenye vyuma chakavu kwa vile tu imekutwa na kutu
“Kwa taarifa zetu za kiintelejensia tulizo nazo ni kwaba silaha hiyo ni moja ya zilizofukiwa na wahalifu lakini wakasingizia kuwa chuma chakavu kwa kuwa ina kutu, taarifa tulizonazo ni kwamba baadhi ya waliokuwa wafungwa na kuachiwa kwa msamaha wa Rais wanahusika na vitendo kama hivi na wamekwenda kufichua silaha ambazo walizifukia ardhini na sasa wanaziibua kwa ajili ya kuzitumia” alisema Mambosasa
Kutokana na taarifa hizo Mambosasa alionya kuwa mtu yeyote ambaye amepata msamaha baada ya kumshukuru mungu na kuachana na uhalifu hatabaki salama
“Tutawaandalia mashtaka na kuwarudisha huko walikotoka , ukipata msamaha kitu cha kwanza ni kumshukuru mungu na kuachana na uhalifu, Hii bunduki ni kwamba imefukiwa chini na si kwamba imeokotwa kwenye vyuma chakavu ka wanavyodai washtakiwa hao”
“Hawa ni waongo na wapo wengine na wapo wengine wanashirikiana na walioko jela wanawatuma walificha silaha wanakwenda kuzichukua na kuanza kuingia nazo mtaani, tuko imara tutawakamata “ alisema Mambo sasa.
Comments